18 September 2012

ZIARA YA JOHN SHABANI MIKOANI NA VIJIJINI YAFANA

 John akiwa katika picha na watoto wa kijiji cha makulu huko mvumi
John Shabani akiimba na kucheza


Katika kuhakikisha Injili ya Yesu inahubiriwa kwa njia ya nyimbo na Neno l Mungu, John Shabani amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika mikoa na Vijiji kadhaa ndani na nnje ya nchi. Pia pamoja na kuimba na Neno pia kutafiti maisha ya watu mbalimbali wakiwemo Vijana, watoto na hata watu wazima wanaoishi katika mazingira magumu. Pia John amekuwa na mkakati wa kuibua na kusaidia watoto na vijana wenye vipaji.
Katika kuhakikisha jamii inafikiwa kwa ukaribu zaidi, John yuko mbioni kukamilisha usaili wa Tahasisi yake ya HOPE TRUST.  Maombi yako yanahitajika ili kukamilisha ndoto na maono haya makubwa.
Moja ya ziara ni ya wiki iliyopita ambayo amezunguka katika mkoa wa dodoma hasa maeneo ya  Mvumi . Mkutano mkubwa uliandaliwa na Kanisa la T.A.G na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo maaskofu na wachungaji kutoka dini na madhehebu mbalimbali. Pia John aliweza kufurahiya na watoto mbalimbali wanaosaidiwa na shrika la kimataifa la Compation katika kijiji cha Makulu
 John Shabani na mkakati wa kusaka na kuibua vipaji vya uimbaji vijijini

 Wachungaji na maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali wakimsikiliza John Shabani

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP