10 January 2013

BAHATI BUKUKU HAJAFA NI MZIMA KABISA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI NA WATU MBALIMBALI WATOA TAMKO KALI



BAHATI BUKUKU  HAJAFA NI MZIMA KABISA
CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI NA WATU MBALIMBALI WATOA TAMKO KALI

 Bahati Bukuku
 Bahati, Rose Muhando na Mwl John Shabani
 Bahati na Jenifer mgendi

Habari za uzushi za kifo cha Bahati bukuku zimewashtua watanzania na watu mbalimbali duniani. Chama cha muziki wa injili Tanzania, kimefanya kazi kubwa ya kukanusha uzushi huo, ukizingatia kuwa Bahati ni kati ya waimbaji wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Injili pia ni kiuongozi katika chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita). Hivyo chama cha muziki wa Injili kimekemea tabia hiyo ambayo imekuwa ikijirudia mara kwa mara. Sisi tunasema hafi mtu na injili inasonga mbele.

Baadhi ya watu waliokemea tabia hiyo ni :

ADDo November  (Mwenyekiti wa chama cha muziki wa injili)
.....Ni Aibu kwa wanaoeneza Maneno ya Uongo dhidi ya Bahati Bukuku, kiukweli Bahati Bukuku ni Mzima wa Afya na nimeongea naye muda si mrefu natoaa wito tuziddi kuwaombea Wanamuziki wa Injili na kuwafunika kwa Damu ya Yesu...!! Hafi Mtu na Injili Inasonga In Jesus Name...!!
John Shabani (Naibu katibu mwenezi wa chama na mwalimu wa muziki wa Injili Afrika Mashariki) Hakika hii si tabia nzuri na tena imekuwa ikijirudia si kwa Bahatati tu, pia hata kwa waimbaji na wasanii mbalimbali nchini. Sisi tunakemea hali hii.
Producer Eck: Hakika habari hizi zilinishtua sana, ukizingatioa ngoma mpya ya bahati ya Dunia haina huruma niliyoitengeneza hapa studio ndio kwanza inafanya vizuri. Hivyo nililazimika kuwasiliana nia kiongozi wa Chama cha muziki wa Injili bwana John shabani, majibu ya shabani yalikuwa kwamba Bahati ni mzima kabisa. Lakini pia ilibidi nimtafute bahati, akaniambia waambie mimi sijafa.
Deborah Harold roho ya mauti haina mamlaka kwa waimbaj wa gospel wote katika jina la yesu aliye hai,amen
 
Rachel Sozigwa hafu kwa nini watu huwa wanajifanya wanajua watu sana na kuwasingizia vitu vya uongo?hata kama umjui mara kaolewa kaachwa anaumwa sana haipendezi loh

Benedicta Mrema N a kwanini umtangulize mwenzio...kama umechoka kuishi tangulia wewe,tuache sisi tufanye kazi tuliyoitiwa KUHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE KWA NAMNA YOYOTE ILE, alaaaaaa!

Mtitu Alex Mdidi Lazima mkubali kuwa tupo duniani na wengi wanaenenda kwa kumfuata mkuu wa anga na matendo yake. Watasema mengi lkn watahukumiwa kuwa ni wakosaji
  Jordan Mwanjala ASANTE MUNGU "NAMI NILIPOSIKIA NILISISTUKA SANA NA IKANILAZIMU NIINGIE FB SIKUKUTA KITU IKABIDI NIWAULIZE IR NA NEG
Jordan Mwanjala NAO AWAJANIJIBU NASHUKURU KWA TAALIFA YAKO MUNGU AMUONGEZE SIKU BUKUKU SAUTI YAKE NZITO IZIDI LINDIMA KTK KUTANGAZA NEN
Jordan Mwanjala NA IWAPO KAMA ANA ANAUMWA MUNGU AMUONDOLEE MAUMIVU AMUONGEZE NGUVU ILI AWEZE KULITANGA NENO LA MUNGU AMINA
Jordan Mwanjala NA IWAPO KAMA ANAUMWA MUNGU AMUONDOLEE MAUMIVU AMUONGEZE NGUVU ILI AWEZE KULITANGAZA NENO LA MUNGU AMINA
Obby Mwakyoma kaka nashukuru.,yatupasa tuombeane uzima na afya tele huku tukilindwa na damu ya yesu
Neema Mkakata mmmh huyo ni shetani tu baba wa uongo anajaribu kupindisha mambo,lkn Mungu mwema awafunike wanamuzik wa gospel ktk damu ya Yesu na roho za umauti.dah niliona jana post moja nilishtuka sana Na nkakosa amani kweli Dunia haina huruma
Thomas Luvanda Aisee afadhali umetufahamisha ukweli maana mm nimepata sms 3 alafu nyingine imenifikia kwamba rose muhando kapata ajali aisee mungu awafunike na kuwalinda roho ya mauti kifo imeshindwa haiwezi kuwapata kwa jina la yesu kristo wa nazaret amen
Bilionear Macdaut Shayo BRO ADDO MI KIUWELI NIMESHTUKA SANA KIASI NILIKUWA NIMEKAAA NILISIMAMA GHAFLA NA ZAIDI KILICHONIUA KABISA NIKAJUA NI KWELI NAFUNGUA REDIO UWAPO NAKUTANA NA NYIMBO YAKE ILE YA DUNIA SINA HURUMA KILICHONISTUA NI UZUSHI NI MTANGAZAJI ALIKUWA ANACHEKA NA ANARAHA NA TENA ANASEMA NASIKILIZA MOJA YA NYIMBO ZA BAHATI HISTORIA YA KWELI ILA ANACHEKA NIKAJUA UONGO ASANTE KWAKULIWEKA HILI KUWA NI UONGO KESHO NITALIKEMEA NIKIWA KWENYE KIPINDI CHANGU PALE ATN TV SIO VIZURI KABISAA BAHATI UBARIKIWE MAMA MUNGU AKUWEKE DAIMA NA UISHI MAISHA MAREFU KABISAA WANAOSEMA WABAKIE MIDOMO WAZI

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP