12 January 2013

UJUMBE WA January 2013 na John Shabani
Mfumo wa maisha ya mwanadamu huwa kama unavyoziona picha hizi;
Kuna wakati wa kuonekana umefifia(upo kama haupo), wakati wa mchoro wako wa kimaisha kuanza kuonekana kwa mbali, wakati wa kuonekana katika rangi nyingine, wakati wa rangi yako ya ki uchumi au kiroho n.k  kuanza kuonekana kwa mbali, wakati wa wewe kung’aa katika rangi yako na baadaye kuchanua.
Picha hizo zinaashiria changamoto mbalimbaliza kimaisha, yawe ya kiroho, kia-afya na ki-uchumi. Katika kila changamoto, usiogope, usikiate tamaa bali zione changamoto kama daraja la kuvukia upande wa pili wa mafanikio yako. Kuna wakati wa kudharauliwa,  kuchekwa, kushushwa chini na kuachwa/kutengwa. Lakini wakati wa kung’aa kwako na baadaye kuchanua utafika tu!
MARUFUKU KUKATA TAMAA

Reactions:

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP