9 January 2013

ECK PRODUCTION, STUDIO BORA TANZANI, WASANII WENGI WAIKIMBILIA



 Producer Eck akiwa kazini
Producer msaidizi BS akiwa kazini
 Producer Eck akipiga Bass Guitar

Unapotaja studio bora na zinazofanya kazi nzuri Tanzania, huwezi kukamilisha horodha bila kuitaja Eck Prtoduction. Studio hiyo ambayo siku za nyuma ilijulikana kama Zoom Production, ilianza kujinyakulia umaharufu pale iliporekodi album ya mwanadada Rose Muhando ijulikanayo kwa jina la UTAMU WA YESU.
Waimbaji wengi na wasanii mbalimbali wa ndani na nnje ya nchi sasa wanafanya kazi zao Eck production. Akizungumza na JohnShabani, Mr.  Enock au kwa jina maarufu Eck ambaye ndiye mmiliki wa studio na producer, alisema kuwa anamshukuru Mungu kuona kwaqmba waimbaji wengi sasa wanafanya kazi zao na kazi zao zinakubalika ile mbaya. Moja ya ngoma iliyobamba vibaya ni ile ya Bahati Bukuku ijulikanayo kwa jina la Dunia haina huruma.
Waimbaji wengine ambao wamefanya kazi nzuri na Eck Production ni John Shabani na album yake mpya  iliyoshirikisha waimbaji nyota na wengine chipukizi kama vile Cosmas Chidumule, Upendo Kilahiro, Jane Misso, Faraja Ntaboba kutoka DRC, Christina Matai, Bella Kombo na wengine kibao. Albamu hiyo mpya ya John Shabani inategemea kuachiwa mwezi ujao ikisimamiwa na kampuni ya Msama Promotion kwa mfumo wa Audio na video. Wengine ambao tayari wamerekodi kazi zao pale Eck production ni Masanja mkandamizaji, Boniface mwaitege, Davi Robert, Stella Joel Akimshikisha Rose Muhando, Upendo nkone, Christina shusho, Addo November, Isaya Msangi, Dr. Mihambo na wengine kibaooooooo!...

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP