14 June 2013

JOHN SHABANI NA UTAMBULISHO WA ALBUM YAKE MPYA


 John Shabani akihojiwa na  mtangazaji wa Upendo Radio, bwana Isack Kikula

Isack Kikula na bi Naomy Kisamo ndani ya Upendo Radio
 


Mr. Isack Kikula wa Upendo Radio akihojiana na Mwl John Shabani kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo muziki wa injili pamoja na Darasa la uimbaji na sauti, pia Kuitambulisha album mpya.
Hakika kipindi hicho cha takriban saa moja, kimekuwa cha Baraka kwa wapenzi na wasikilizaji wa Upendo Radio. Hakika nimepokea simu nyingi kutoka ndani na nnje ya nchi pamoja na mialiko ya kuzungukia kwaya na vikundi mbalimbali, ili kutoa elimu ya sauti na uimbaji, kusaidia vikundi vya kusifu na kuabudu pamoja na waimbaji wengi kuniomba niwatungie nyimbo.
Mungu wabariki watangazaji wote na uongozi wa Upendo Radio.
Darasa la sauti na uimbaji linaendelea kesho saa 9-12 pale kinondoni studio na jumapili saa 8-10 katika ukumbi wa chuo cha Ustawi wa Jamii sinza bamaga. Mawasiliano: 0716560094

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP