28 October 2013

MTANDAO WA WANA MUZIKI TANZANIA WAFANYA WARSHA YA SIKU MOJA JIJINI DAR ES SALAAM


 Mwalimu john shabani ndani ya warsha hiyo






Picha ya pamoja na naibu katibu mkuu, wizara ya habari, utamaduni na michezo

Mwenyekiti wa mtandao wa wanamuziki Tanzania, akifafanua jambo mbele ya wana muziki kutoka makundi  mbalimbali ya muziki na wadau wa muziki, katika kujadili mambo mbalimbali likiwemo mustakabali mzima wa mwenendo wa muziki na wana muziki wa Tanzania. Mengi yamejadiliwa na mwisho, aliyekuwa Mgeni rasmi katika Warsha hiyo Naibu katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, ametoa pongezi za dhati kwa wote waliofanikisha Warsha hiyo; akianzia na uongozi wa Mtandao wa wana muziki tanzania (Tanzania Musicians Network), BEST – AC (The Business Environment Strengthening in Tanzania) ambao ndio waliodhamini warsha pamoja na mshikamano walioonyesha wasanii kutoka makundi mbalimbali.


Pia Kiongozi huyo wa serikali Mheshimiwa Sihaba Nkinga, amewashauri wasanii kuamka na kwenda na wakati, Kufanya kazi kibiashara, kufikiria kibishara na kupata taaluma ya biashara.

Amezizungumzia fursa mbalimbali zilizopo kwa sasa na mikakati inayopangwa ili kuwasaidia wasanii wa kitanzania.

Warsha hiyo iliofanyika katika mgahawa wa kisasa wa Nyumbani, imehudhuriwa na wasanii kutoka makundi mbalimba huku upande wa Injili ukiwa umewakilishwa na mwalimu John Shabani na Sifa John. Vyombo mbalimbali vya habari vimehusika kuchukuwa habari.
Kwa pamoja tutafika

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP