5 May 2014

RULEA SANGA APENDEKEZA JJ BARBER SHOP KUWA KITUO CHA WAPENDWA KUFANYA MAHOJIANO

 John Shabani akiwa anepumzika kidogo ndani ya JJ Barber shop baada ya kushinda kutwa nzima akiwasimamia mafundi.

Huyu ndiye rulea sanga, hapa alikua akiwa ndani ya ndege kuelekea Nigeria kwa mwaliko wa Mtumishi mkubwa wa Mungu, TB Joshua

Baada ya siku chache, nilipoweka facebook picha za matengenezo yanayoendelea ya salon ya kisasa "JJ Barber shop", moja ya watu walionifurahisha katika jumbe zao ni bwana Rulea sanga (Mkurugenzi wa Rumaafrica na mmiliki wa blogu: www.rumaafrica.blogspot.com); huu hapa ujumbe wa Rulea:
"Broda Gog bless you..Tutaanzisha kipindi cha TV na hapo patakuwa center kwa wapendwa kufanyia mahojiano..Wazo langu kwako..Tumuunge mkono mpendwa wetu"

Nimeguswa sana na moyo huu wa kutakiana mema. Huu ndio upendo aliousema Yesu alipokua akiondoka. Nimekua nikiumia sana ninapoona wana wa Mungu wakibaguana, kuoneana wivi na vijicho, roho ya ubinafsi, makundi, roho ya tukose wote. Ebu tushikamane, tutiane moyo, tulie na wanaolia, tufurahi na wanaofurahi. 

Mimi nayakaribisha mawazo yoyote yanayojenga na kuifanya JJ Barber shop kuwa ya mfano wa kuigwa. Nawakaribisha rafiki zangu watangazaji wa redio na Tv za injili kufanyia mahojiano yao hapa huku wakupulizwa na kiyoyozi na kutengeneza uso, nywele, kucha na hata kuoshwa miguu n.k


 

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP