26 July 2014

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI CHASABABISHA DAR ES SALAAM- JANUARY MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANAMUZI WA MUZIKI WA INJILI NA WASAMBAZAJI NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOHUSIKA NA MUZIKI TANZANIA





Katika kikao hicho Mh. Januari Makamba aliweza kutoa hutuba ndefu yenye ufasaha kwa wanamuziki wa Injili Tanzania. Hotuba yake ilikuwa na matumaini kwa wanamuziki na iliweza kuwafurahisha sana wanamuziki hawa hasa pale alipoweza kutoa ahadi zake za kukisaidia Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania ikiwemo kuwaahidi kuchangia katika kufanikisha zoezi la kuwa na Channel ya TV ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, kuwa na studio ya kisasa itakayomilikiwa na chama cha muziki Tanzania, kufikia suala la kupata eneo la kuendeshea shughuli zao n.k. Aliomba sana wanamuziki kuwa na nguvu za bidii za kuweza kufanikisha yale yote yanayowazunguka na wasibweteke wakisubiria, na pia wanamuziki wa injili wanategemewa kuwa kioo na mfano wa kuigwa, hivyo wawe na nidhamu na uchaji wa Mungu na kujiepusha na skendo, maana nyimbo za injili zinapendwa na kila mtu hata wapagani na wale wa dini zingine. Pia ameahidi kutekeleza ahadi zake haraka iwezekanavyo

 Wadau wa muziki wa Injili wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Shirikisho la Muziki wa Injili John Shaban akiendesha mkutano.

 Kiongozi wa mtandao wa wanamuziki Tanzania, mzee John Kitime

 George Mpella akiwakilisha vyombo vya habari vya kiristo

 Kutoka TRA

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Doreen Sinare (kulia), akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimba kwa wadau wa muziki wa Injili. Wa pli kulia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho.

 Watu mbali mbali wakiuliza maswali

 Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado Novemba (kushoto),  akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanzania Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam  kabla ya kumakribisha mgeni rasmi wa mkutanmo huo, Mhe. January Makamba.

 Balozi mstaafu, Profesa Coster Mahalu akizungumza na wadau wa muziki wa nyimbo za Injili. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kinondoni Revival Choir, Dk. Jotham Mackenzie





Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatiliamambo mbalimbali.
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo.
 

 Wawakilishi wa ATN (Agape Television Network)


Kiongozi CHAMUITA  kutoka Morogoro akikabidhi MIC baada ya kujitambulisha
Muwakilishi kutoka ATN akijitambulisha


 John Shabani akihakikisha kila kitu kinakaa sawa




 Wadau wa eneo la  usambazaji wa kazi za wanamuziki wakiwa kwenye mkutano huo




  Mwanahabari wa Kituo cha TV 1, Gervas Mwaitebela naye alikuwepo kupata taarifa za mkutano huo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (kulia), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanaznia Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam leo.














0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP