22 July 2014

PAMOJA NA KEBEI NA KUZOMEWA MCHUNGAJI STELLA AENDELEA KUHUBIRI INJILI

 Mchungaji Stella Mahiga akiendelea kuchapa injili maeneo ya k/koo
Huku akiendelea kuhubiri, huku akizomewa na kundi la watu

Mhubiri wa Injili ambaye ni mama aliyejitambulisha kwa jina la Stella Mahiga amejikuta akipata wakati mgumu alipokuwa anahubiri majira ya jioni katika kituo cha kupandia daladala kilichopo Kariakoo jijini Dares salaam.
Aidha, mhubiri huyo aliyekuwa anahubiri kuhusu wokovu amejikuta akizomewa na watu aliokuwa akiwahubiria injili katika eneo hilo. Asilimia kubwa ya watu walikuwa katika hilo walikuwa ni wa dini nyingine.
Mpaka mwandishi wetu anaondoka katika eneo hilo aliacha wananchi wakiwa wanamzomea mhubiri huyo kwa maneno ya kejeli. Kwa ujumla hajapata ushirikiano hata kidogo kutoka eneo hilo, lakini Neno litaendelea kuhubiriwa.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP