26 July 2012

Hali ya mwimbaji wa The Voice, Obed Mark yaendelea kuhimarika




Mwimbaji wa kundi la muziki wa injili wanandugu, The Voice, Obed Mark aliyepata ajali ya Bajaj hivi karibuni maeneo ya Sinza, Kamanyola, anaendelea vizuri kwa msaada wa Mungu.
                                                                          Obed Mark
Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi hilo, Josiah Sadock, aliwashukuru mashabiki na wadau wote waliokuwa wakimuombea mwenzao huyo apone haraka.
"Obed anaendelea vizuri, tunashukuru Mungu

Aidha katika ukurasa wao wa Facebook, ThevoiceTZ waliandika kuwa mwenzao anaendelea vizuri hivyo wazidi kumuombea na bila shaka dawa alizopewa zitamsaidia apone haraka na kurudi katika hali yake ya awali. The Voice, wanatarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha la LOVE TANZANIA with Andrew Palau hapo Agosti 11-12.

Nikiwa mwimbaji wa injili pia kiongozi katika chama cha muziki wa injili Tanzania, pamoja na kutoa mchango, pia nawahamasisha waimbaji wenzangu, wachungaji na kila mdau wa Muziki wa Injili tumsaidie mwenzetu katika wakati huu mgumu. Nawashukuru wote wliojitokeza kumchangia, pamoja na vyombo mbalimbali vya Injili vikiongozwa na Praise Power Radio kwa kuhamasisha

Uongozi wa blogu hii unamuombea Obed apone haraka ili arejee kujiunga na wenzake mapema!

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP