4 July 2012

JE! WATANGAZAJI MAHIRI WAPRAISE POWER KUREJESHWA REDIONI??NI HARRIS KAPIGA (HK 1), HUDSON KAMOGA (HK 2), IKUPA NGAO, ANNA NELSON, FURAHA MASINGA NA ELIZA ULOMI.






Watangazaji Mahiri Walioileta Radio Bora Kabisa ya Praise Power FM katika Anga la Habari na Kuwa Radio inayosikilizwa sana na Wakristo akiwepo Harris Kapiga, Hudson Kamoga, Eliza Ulomi, Ikupa Ngao, Anna Nelson, Onesmo Nguse pamoja na Furaha Masinga Kurudi tena Kwenye Radio hiyo???

Hii ni baada ya kusikia  Tangazo kupita Praise Power likiashiria kuwa Kikosi Kazi hicho kinarudi tena Mjengoni kwa ajili ya Kuirejesha Radio hiyo Katika graph zake za Zamani baada ya Radio hiyo Kupoteza Umaarufu wake siku za hivi Karibuni.

Tayari katika kipindi cha Rise and Shine Majembe Mawili HK 1 na HK 2 yaani Harris Kapiga na Hudson Kamoga Wamesikika hewani wakienda Sambamba na Wasikilizaji

Watangazaji hao ambao mpaka sasa Wanaendelea Kusikika hewani wameonesha "Ukongwe" wa hali ya juu katika kuwasilisha habari katika Radio hiyo, Pastor Harris Kapiga ambaye Kwa Sasa ni Mtangazaji wa Radio Bora kabisa Clouds FM na Hudson Kamoga ambaye anamalizia Masomo yake Ya Shahada Ya Habari Chuo Kikuu wameleta Matumaini Mapya katika Radio hiyo.
Habari tulizozipata ni kwamba watangazaji hao wataanzakusikika. Watangazaji wa Kike Ikupa Ngao na Furaha Masinga ambao enzi hizo Walikuwa wakitangaza kipindi Cha "Kona Za Praise Power". Ikupa Ngao ambaye Kwa sasa yuko Trinity na Furaha Masinga ambaye yuko TBC 1 wataleta radha tofauti mida hiyo ya Asubuhi.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP