30 July 2012


TANGAZO KWA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI
Wasanii wote wa nyimbo za injili, Dansi, Taarabu na Bongofleva, kwa msaada au kupitia ofisi ya sheria (TRUSTWORTH ATTONEYS) wameombwa kufuta mikataba yote RINGTONES na CALLERTUNERS walioingia na mitandao ya simu. Pia makampuni mbalimbali yanayojihusisha na nyimbo za wasanii yameandikiwa barua za kufuta  mara moja mikataba ya kutumia nyimbo na muziki wa wasanii, pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi za wasanii kwa njia ya  Tlevision, radio, Magazeti, Blogs, Website na ujumbe mfupi wa maneno wa kwenye simu kupitia mitandao tofauti.
Hii ni kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kurejesha heshima ya wasanii na kazi zao. Ukweli ni kwamba, wasanii nchini hawanufaiki na kazi zao kama inavyostaili.
Kwa waimbaji wote wa nyimbo za Injili ambao tayari wamejiunga na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kutumia nyimbo zao kama milio ya simu au miito ya simu, wanaombwa majina yao na kampuni walizoingia mikataba ili kuorodheshwa na kuweka sahihi ya kuvunja mikataba, ili kutafuta njia sahihi ya kuingia mikataba na kunufaika na kazi zetu.
Kwa mawasiliano zaidi : E-mail: touchingvoice@yahoo.com, Mob: 0754818767

Hapo juu ni moja ya barua zilizoandikiwa makampuni  mbalimbali yanayojihusisha na kazi za wasanii.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP