17 June 2014

MUME MWEMA NI YUPI?

Ni maswali ambayo majibu yake yana utata mwingi, wengine wakidhani kuwa wamepata mwisho wa siku ni majuto, na wengine wakionekana kuwa ndivyo sivyo kumbe wamepatia...


Swali langu ni hili:
Hivi unapoomba Mungu akupe mume mwema, una maanisha nini?
Je ni mume ambaye anajali familia pia ana upendo kwa familia yake? Ni msomi, mwenye kipato kizuri, mtanashati au aliyeshikilia dini sana au mtu wa sala? . Mungu anajibu maombi kwa aina nyingi sana lakini wanadamu huwa tunapingana na mpango wa mungu

Mume mwema hatoki kwa ATM ao sio awe kama ATM eti ndo mume mwema , mume mwema sio muonekano ao kuwa anamilika nyumba, magari, kazi ya juu, ao kabila . Tumeshuhudia mara nyingi watu walikimbilia kuolewa na masupasta, matajiri au vijana watanashati lakini mwisho wake ni vilio, na wengine kupelekana kaburini. Sijapinga  suala la kuwa na chagua la aina ya mwenzi unayemtaka, lakini Mungu apewe nafasi ya kwanza katika maamuzi

Ebu angalia picha hii jinsi wanavyopendeza.
kila mtu  vyovyote vile alivyo anaweza kuwa mume mwema!...

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP