20 June 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI DEBORA SAID AFARIKI DUNIA



Mama Askofu, mwimbaji wa injili na mjumbe wa chama cha muziki wa injili, debora John Said hatunaye tena kimwili!...
Gospel in Africa imepokea kwa masikitiko makubwa sana juu ya kifo cha Debora, tunawapa pole wafiwa na Watanzania wote na kupotelewa na mtumishi wa Mungu na kipenzi cha wengi, mama Askofu John Said, mwimbaji na mjumbe wa chama cha muziki wa Injili Tanznzania, ambaye amefanya kazi yake kwa upendo na uaminifu. Mungu azidi kuipigania familia  na wale wote waliokuwa wakimtegemea kiroho na kimwili. Ni wakati wa waimbaji wa nyimbo za injili kujifunza jambo, kurudiaha umoja na upendo aliotuachia Yesu. Sisi tuliobaki tuzidi kumtumikia Mungu kwani hatujui vilivyombele yetu.
 Huu ni wakati wa kuungama na kutubu makosa tunayoyafanya katika maisha yetu hapa duniani. Mungu amekupa kipaji fulani kwa kazi yake basi kitumia na usiache. Debora amefanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji kwa umaminifu mwingi, bila skendo, bila majivuno wala majigambo, amekuwa ni mshauri mzuri, hakuwa na wivu kabisa, na sasa ametangulia.

IBADA YA KUMUAGA ITAFANYIKA JUMATATU SAA NNE ASUBUHI KATIKA KANISA LA MAISHA YA USHINDI MABIBO EXTERNAL NA BAADAYE SAA NANE MCHANA MAZISHI KATIKA MAKABURI YA MABIBO JESHINI.

John Shabani
Katibu chama cha muziki wa injili Tanzania

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP