11 June 2012

JOHN SHABANI AGUSA MIOYO YA WATANZANIA, TAMASHA LAKE LAWA LA KIHISTORIA

John shabani akimsindikiza Mheshimiwa Fenella Mukangara 
(Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na michchezo)



Tarehe 10.06.2012, imebaki kuwa siku ya historia kwa maelfu ya watu katika jiji la Dar es salaam na Tnzania kwa  ujumla. Ni lile  tamasha la kusifu na kuabudu pamoja na maombi maalum kwa ajili ya nchi ya Tanzania, ambalo liliandaliwa na mtumishi wa Mungu John Shabani .
Katika tamasha hili mgeni rasmi alikua  Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo, Mh Dr Fenella Mukangara.Mh Mukangara baada ya kuzindua DVD na BLOG ya John Shabani, pia ameongoza harambee ya kuchangia huduma ya mtumishi huyo wa Mungu

Mamia Ya Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam   walijitokeza kwa Wingi Katika Tamasha hilo ili Ku-m-Support Mwanamuziki Nguli wa Muziki wa Injili John Shabani lililofanyika Katika Kanisa la TAG Magomeni.

Moja kati ya matukio muhimu katika tamasha hili linaloendelea hapa ni uwepo wa wakongwe wa injili nchini Mzee makasi, Mzee Cosmas Chidumule.Pamoja na hayo Upendo Kilahilo pamoja na Stara Thomas aliye okoka hivi karibuni.  John Shabani, Upendo Kilahiro pamoja na Apostle John Komanya walipanda jukwaani na kuimba kwa pamoja wimbo wa tenzi uitwao KALE NILITEMBEA  amabao kimsingi umegusa mioyo ya wengi. Wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo kali zilizomo katika albam mpya ya John Shabani, Album hiyo inasimamiwa na Kampuni ya Msama Promotion na inategemea kuwa tayari muda si mrefu. Nyimbo zingine zilizomo katika album hiyo ni pamoja na
Kwa Yesu kuna raha – John Ft Cosmas Chidumule
Tunaye Baba – John Ft Jane Misso
Wewe ni Baba – John Ft Faraja Ntaboba (DRC Kongo)
Mungu yu mwema – John ft. Christina Matai
Nimemwona Bwana – John ft. Tina Marego
Akisema Ndio – John ft. Destiny Sisters (Kampala)
Wakati wangu – John ft. Bella Kombo


Katika tamasha hili rangi iliyotawala ni Red kama ionekanavyo pichani na pia  limehudhuriwa na Rais wa waimbaji nchini Mtumishi Addo November. Waimbaji wengi pamoja na kwaya na vikundi mbalimbali wamehudhuria katika tamasha hilo. Pia waandishi mbalimbali wa habari na vyombo mbalimbali vya habari vikiongoza na Television ya taifa TBC vilikuwepo. Maombi maalumu kwa ajili ya Nchi yetu yameongozwa Na Mchungaji Danstan Kanemba pamoja na Bishop Rechael.

 John Akiimba kwa hisia


 John Shabani akiagana na Mheshimiwa Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo


 Cosmas Chidumule na Stara Thomas


Bloggers wakiwa Kikazi zaidi siku ya Leo, Kushoto ni Victor, Kati ni Papaa Ze Blogger na Kulia ni Tunu wakiwa Kikazi zaidi siku ya Leo.




 Mzee Makasy, mkongwe wa muziki Afrika

 

 John Shabani, Bishop John Komanya kushoto na kushoto ni Upendo Kilahiro ndani ya Tamasha


Victor Ahron na Rais wa Shirikisho la muziki Tanzania, mr. addo November
 


 Martin Malechela, Addo November pamoja na Uncle Jimy





 John Shabani na kundi lake wakifanya mambo

 Watu weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Haya sasa, Hayo ni Mambo ya Yesu 

1 comments:

Mary Damian said...

Kazi njema sana..wa utukufu wa Mungu!

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP