6 June 2012

STARA THOMAS KUSHUSHA UWEPO WA BWANA KATIKA TAMASHA LA SIFA NA KUABUDU LILIANDALIWA NA MWL JOHN SHABANI.





Baadada ya kuamua kumtumikia Bwana na kutoa Albam yake ya kwanza ya injili iitwayo NANI NI MSHABA, sasa jumapili hii. katika kanisa la TAG magomeni, atakuwepo akiungana na waimbaji wa injili kusmsifu Mungu siku hiyo.

Mgeni Rasmi Dr. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, karibu na Hoteli ya Travetine, tarehe 10.06.2012
Viongozi mbali mbali wa Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali na madhehebu ya dini, wakiwemo Mheshimiwa Rev. Dk. Getrude Rwakatare, Eng. Juliana Palangyo, Mheshimiwa Martha Mlata (MB), Mheshimiwa Dk. Mary Mwanjelwa (MB), na wengine wengi wamethibitisha kuhudhuria.

Mheshimiwa Mbunge Martha Mlata ataimba pamoja na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kama vile Mzee Makasy, Cosmas Chidumule, Stella Joel, Safi kutoka Rwanda, Faraja Ntaboba kutoka Kongo, Upendo kilahiro, Christina Shusho, Addo November, Joybringes kwaya, Revival kwaya ya T.A.G Magomeni, Albino group na wengine wengi.

Kwamawasiliano zaidi: 0713 778 778

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP