4 June 2012

MSAMA KUWA MIONGONI MWA WAGENI MAALUM KATIKA TAMASHA LA KUMTUKUZA MUNGU BABA NA KULIOMBEA TAIFA LETU



 Msama katika harakati za kusaka maharamia wa kazi za sanaa Tanzania

 Msama akiwa na Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri ya muunganao wa Tanzania
                               Dr. J.K Kikwete

Mmoja wa mapromota maarufu wa muziki wa injili afrika mashariki na mkurugenzi wa makampuni ya msama promotions, Mr Alex msama, ni miongoni mwa wageni maalum watakao hudhuria katika tamasha la kumtukuza Mungu Baba pamoja na maombi maalumu kwa ajili ya nchi yetu.

Msama ambaye pia ndiye meneja wa mwalimu John Shabani, amethibitisha kuwepo katika tamasha hilo, ili kuwatia moyo waimbaji na pia kuungana na mheshimiwa Mgeni Rasmi Dr. Fenella Mukangara, Waziri wa Hahari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, karibu na Hoteli ya Travetine, tarehe 10.06.2012
Viongozi mbali mbali wa Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali na madhehebu ya dini, wakiwemo Mheshimiwa Rev. Dk. Getrude Rwakatare, Eng. Juliana Palangyo, Mheshimiwa Martha Mlata (MB), Mheshimiwa Dk. Mary Mwanjelwa (MB), na wengine wengi wamethibitisha kuhudhuria.

Mheshimiwa Mbunge Martha Mlata ataimba pamoja na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kama vile Mzee Makasy, Cosmas Chidumule, Stella Joel, Safi kutoka Rwanda, Faraja Ntaboba kutoka Kongo, Upendo kilahiro, Christina Shusho, Addo November, Joybringes kwaya, Revival kwaya ya T.A.G Magomeni,  Albino group na wengine wengi.

Katika tamasha hilo Mr Msama atatoa nasaha kwa waimbaji pia jinsi alivyojipanga kutokomeza maaramia wa kazi za sanaa nchini na kuinua vipaji vya wasanii.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP