23 June 2012

MWL JOHN SHABANI MA HARAKATI ZA KUIBUA VIPAJI VYA WATOTO NA VIJANA (JOHN SHABANI WITH CHILDREN AND YOUTH TALENT SEARCH)

John Shabani katika harakati za kuibua vipaji



Familia na watu mbalimbali wamekuwa wakifika katika kituo cha kuibua vipaji vya watoto na vijana hasa kupitia uimbaji. Mafunzo hayo yanaongozwa na kusimamiwa na mwalimu wa muziki wa Injili Afrika mashariki, bwana John Shabani.

Moja ya familia zilizofurahishwa na mpango huo wa John Shabani ni ile ya Cornel au Kazinja Family maarufu kama familia ya mama wa kihindi. Tayari watoto wa familia hiyo wameendelea kufanya vizuri katika uimbaji chini ya Mafunzo ya John shabani, na baada ya siku chache watapelekwa studio kwa maandalizi ya kurekodi mkanda wa audio na Video.

Mpango huo wa mwl John umepongezwa na mamia ya watu akiwemo Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara; ambaye hivi karibuni alikua mgeni Rasmi katika tamasha lililoandaliwa  na John Shabani.

 John Shabani na mazoezi ya pumzi
John Shabani na Tanzania Gospel All stars 
katika maandalizi ya wimbo maalum wa miaka 50 ya
uhuru wa Tanzania mwaka jana



0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP