14 June 2012

MASANJA MKANDAMIZAJI AACHIA DVD YAKE YA GOSPEL MTAANI HII LEO



Hatimaye yule mchekeshaji maarufu nchini bwana Emanuel Mgaya ama mwite Masanja Mkandamizaji wa kundi la vichekesho la Original Comedy hii leo ameachia mtaani DVD yake ya kwanza ya gospel iitwayo ''Hakuna jipya'' ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake pamoja na wapenzi wa muziki wa injili nchini, kutokana na ujumbe uliomo kwenye nyimbo zake.

Album hiyo yenye nyimbo tisa, imerekodiwa maeneo tofauti nchini na nje ya nchi ambapo kazi ya kurekodi ilichukua muda mrefu na sasa imekamilika, ambapo audio yake kwa walioisikia wameikubali hasa uimbaji wa wawaitikiaji ambao wana sauti zilizojaa na mvuto huku Masanja mwenyewe a.k.a mchungaji mtarajiwa akijazia kwa mashairi mbalimbali ambayo licha ya mafunzo mazito pia inakuachia vicheko na tabasamu ikiwemo wimbo uliobeba album wenye maneno aliyochombeza kama Mungu akang'oa koki ya bomba mvua ikanyesha .... na maelezo mengine mbalimbali

Mwimbaji na mchekeshaji huyu pia anaimba kwaya ya New Jerusalem Choir (Watoto wa mito ya baraka) ya kanisa la E.A.GT Mito ya baraka lililochini ya askofu Bruno Mwakiborwa likiwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam karibu na jengo la klabu ya soka ya Yanga.Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Hakuna jipya, Nimemchagua, Maisha yangu, Chapa mwendo, Hili nalo litapita, Amini,Zaburi ya 150, Busy pamoja na Wadogo zangu(maalumu kwa watoto).

Kitu ambacho amewahi kuwachekesha watu kuhusiana na album yake hiyo, Masanja alisema anaruhusu wezi wa kazi za waimbaji kuiba watakavyo kwani wanamsaidia kutangaza injili na kumtangaza zaidi kwahiyo ikawa kama ametoa ruksa kwa wale wezi, jambo ambalo ni tofauti kwa waimbaji wengine ambao wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao kila leo.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP