1 May 2012

LET US PRAY FOR NIGERIA (TUIOMBEENIGERIA, HALI SI SHWARI MCHUNGAJI NA WAUMINI WAKE WAULIWA NDANI YA KANISA,WENGINE WAFUNGA MAKANISA)



 Baadhi ya miili ya watu waliochomwa moto ndani ya jengo la kanisa.

Ombi limetolewa na mchungaji Yuguda Mburnvwa wa kanisa la Church of Brethren la  nchini Nigeria kuwaombea Wakristo wanaoishi kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na mauaji yanayofanywa na wapiganaji wa kikundi cha kiislamu kiitwacho Boko haram dhidi ya wakristo wa nchi hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na kituo cha Premier radio ya kikristo nchini Uingereza,mchungaji Yuguda amesema waumini wapatao 16 wameuwawa katika jimbo la Kano ambapo kwa mujibu wa vyanzo vya ulinzi vimesema watu wenye bunduki wakiwa kwenye pikipiki walirusha bomu ndani ya ukumbi wa chuo kikuu ambao unatumika kufanyia ibada na kuwafanya waumini kukimbia huku watu hao wakiwamiminia risasi na kuwaua.

Kutokana na hilo makanisa mengi kaskazini mwa nchi hiyo yamefungwa waumini wanaogopa kwenda kuabudu kutokana na vitisho pamoja na mauaji yanayofanywa na kundi hilo.Amesema katika shambulio lililopangwa lilisababisha mchungaji mmoja wa kanisa la Church of Christ kufariki dunia pamoja na waumini wake wanne wakati wakiwa kwenye ibada katika jimbo la Maiduguri lililopo kaskazini mwa nchi hiyo ambapo hakuna kundi lililojitokeza kuhusika na mauaji hayo ingawa tukio hilo halina tofauti na matukio mengine ambayo yamekuwa yakifanywa na kundi la Boko haram.

Mchungaji mwingine aitwaye Fred Williams ameiambia Premier kwamba alikuwa akiongoza moja ya makanisa lakini kutokana na mapigano pamoja na mauaji namba ya waumini imekuwa ikipungua kila leo ingawa licha ya hayo kutokea kikundi hicho hakitaweza kuuondoa Ukristo eneo hilo.Ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu watu 450 wamefariki dunia.

Nchi ya Nigeria imejigawa kwa upande wa kidini ambapo Wakristo wengi wapo kusini mwa nchi hiyo huku waislamu wakiwa wengi kaskazini mwa nchi hiyo,kundi la Boko haram ambalo lilitangaza vita na serikali ya jimbo la kati la nchi hiyo,limekataa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yameitishwa na serikali kwa madai ya kutaka wafuasi wao wanaoshikiliwa kuachiwa huru,ikiwa ni pamoja na kutambuliwa kwa sheria zao za kiislamu nchini humo.

                                         Kanisa likiwa limeteketea kwa moto.
Baadhi ya wanawake wakilia kwa uchungu baada ya kupoteza ndugu na jamaa kwenye mauaji yanayofanywa na kundi la Boko haram.




0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP