Baada ya kufanya vizuri
katika kuwaongoza waimbaji wa injili nchini kuimba wimbo maalum kwenye
maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, mwalimu wa John Shabani chini ya udhamini na
usimamizi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania, ameandaa tamasha la kipekee
lijulikanalo kama WORSHIP HOUR (SAA YA KUABUDU) ni saa maalum
ya sifa na kumwabudu Mungu live itakayoongozwa na mass choir chini ya mwalimu
John Shabani, aliyeongoza waimbaji wa injili kuimba katika maadhimisho ya miaka
50 ya uhuru pamoja na waalimu wengine. Pia kutakuwa na muda maalum wa kumshuku
Mungu kwa amani aliyotupa pamoja na kuombea Baraka kwa ajili ya nchi yetu.
Maombi hayo yataongozwa na Dk Getrude Rwakatare.tamasha hilo litaaambatana
na uzinduzi wa Video na tovutiya ya Mlm john shabani.
Kabla ya saa ya kuabudu, Tumealika waimbaji
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Watakao mtumikia Mungu kwa mjia ya
uimbaji. Siku hiyo Mheshimiwa Mbunge Martha Mlata ataimba pamoja na waimbaji
mbalimbali wa nyimbo za Injili kama vile Mzee Makasy, Cosmas Chidumule,
Jangalason, Stella Joel, Safi kutoka Rwanda, Belle Kombo, Celine Theophil,
Mwana mapinduzi group, Faraja Ntaboba kutoka Kongo, Upendo kilahiro, Addo
November, Joseph Nyuki, Albino group na wengine wengi pamoja na kwaya
mbalimbali alizowahikufundisha Mlm John Shabani, na wengine wengi.
Viongozi mbali mbali wa Serikali na mashirika
yasiyokuwa ya serikali na madhehebu ya dini, wakiwemo Mheshimiwa Rev. Dk.
Getrude Rwakatare, Eng. Juliana Palangyo, Mheshimiwa Martha Mlata (MB),
Mheshimiwa Dk. Mary Mwanjelwa (MB), watakuwepo.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi
wa kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, karibu na Hoteli ya Travetine,
tarehe 10 .06. 2012 siki ya jumapili kuanzia saa nane mchana. Hivyo basi,
kwa wale wanaotaka kujiunga na mass choir kwa ajili ya kumtuku Mungu siku hiyo,
wawasiliane na kamati ya tamasha hilo, ili mjulishwe siku za mazoezi na maali
pa mazoezi.
Mawasiliano:
Mob: 0716560094, 0754818767
Web: www.johnshabani.blogspot.com
Vazi la siku hiyo, ni rangi nyeupe na nyekundu
Kuhusu mgeni rasmi, mtajulishwa baadaye. Ila ni mheshimiwa waziri katika serikali yetu.
Tangazo limetengenezwa
na Rulea Sanga +255 715 85 15 23 | www.rumaafrica.blogspot.com |
rumatz2011@yahoo.com
TUNAHITAJI MAOMBI
NA USHAURI WENU
0 comments:
Post a Comment