25 May 2012

MHESHIMIWA DK FENELLA MUKANGARA KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA KUABUDU NA MAOMBI KWA TAIFA

 Dr. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 
Dk/Rev. Getrude Rwakatare

Mh. Martha Mlata (MB)
Tarehe 10.06.2012, ni siku ambayo kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi kwa pamoja wataungana  katika kumsifu na kumwabudu Mungu, sambamba na kuliombea Taifa letu la Tanzania. Dk/Rev. Getrude Rwakatare ndiye atakayeongoza maombi hayo. Pia Maaskofu mbalimbali, wachungaji, vingozi mbalimbali wa serikali pamoja na taasisi zisizokuwa za serikali, wamethibitisha kuwepo siku hiyo.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo, Dr. Fenella Mukangara

Pamoja na kuliombea taifa, pia tovuti pamoja na mkanda wa video ya mwalimu wa muziki wa injili Afrika mashariki, bwana John Shabani vitazinduliwa. kabla ya saa maalumu ya sifa na kuabudu live, waimbaji mbalimbali wakiongozwa na Mh. Martha Mlata wataimba. Wengine ni Mzee makasy, Cosmas Chidumule, Jane Miso, Stella Joel, Faraja Ntaboba, Addo November, Albino Group, Calvary, Nicolina msungu, Bella Kombo, Celine Theophil, Joybringers Choir na wengine wengi. Tamasha litafanyika ndani ya jengo la kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, kuanzia saa saba mchana.

Sambamba na wageni mbalimbali, Pia tumemwalika Mr Ruge Mutahaba, Mr Alex Msama pamoja na viongozi wa Chama Cha Muziki Wa injili Tanzania.

Vazi la tamasha ni rangi nyeupe na nyekundu.

Tunahitaji mchango wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hilo la kipekee.

Usipange kutokuhudhuria siku hiyo.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP